MigogoroUlaya
Watu 12 wauawa nchini Ukraine kufuatia mashambulizi ya Urusi
8 Machi 2026
Matangazo
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amelaani mashambulizi hayo akisema Moscow haijaachana na nia yake ya kuisambaratisha Ukraine, huku akitoa wito wa kuwepo jibu la kimataifa akisema Urusi inaendelea kulenga makazi ya raia pamoja na miundombinu ya nishati.
Zelensky amesema pia kuwa amezungumza hapo jana na Mfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman kuhusu hali inayoendelea Mashariki ya Kati na akapendekeza kutoa msaada wake wa kitaalamu wa namna ya kukabiliana na droni za Iran za Shaheed ikiwa nchi yake pia itaahidiwa msaada kukabiliana na Urusi. Mapema wiki hii, Zelensky alizungumza pia na viongozi wa Bahrain, Jordan, Kuwait, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu.