Watu 10 wauwawa nchini Syria | Matukio ya Kisiasa | DW | 06.08.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Watu 10 wauwawa nchini Syria

Kiasi ya watu 10 wameuwawa baada ya vikosi vya usalama kuwashambulia waandamanaji nchini Syria.

default

Vifaru mjini Hama

Wanaharakati nchini Syria wanasema kiasi ya waandamanaji 10 waliuwawa hapo jana baada ya vikosi vya usalama kuwashambulia waandamanaji waliokusanyika baada ya sala ya Ijumaa. Waandamanaji walimiminika mitaani, kupinga matumizi ya nguvu ya serikali kukandamiza vuguvugu maarufu la katika mji wa Hama.

Jumatano iliyopita, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililaani ukiukaji wa haki za binadamu unaozidi kufanywa na serikali ya Syria pamoja na matumizi ya nguvu dhidi ya raia. Zaidi ya watu 100 waliuawa wiki hii katika mji wa Hama, katika machafuko yanayoendelea kati ya wapinzani wa serikali na vikosi vya usalama vya Rais Bashar al Assad.

Mwandishi: Sudi Mnette

Mhariri: Prema Martin

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com