Watoto wajeruhiwa kwenye shambulizi la anga, Libya. | Matukio ya Afrika | DW | 08.10.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Watoto wajeruhiwa kwenye shambulizi la anga, Libya.

Watu sita wakiwemo watoto, wamejeruhiwa katika shambulizi la angani Libya na kuibua shutuma.

Kiasi watu sita ikiwa ni pamoja na watoto wamejeruhiwa katika shambulizi la angani na kuibua shutuma kali kutoka kwa Umoja wa Mataifa na serikali ya kitaifa.

Mfanyakazi mmoja wa kiafrika alikuwa miongoni mwa waliojeruhiwa katika shambulizi hilo la juzi Jumapili katika kitongoji cha Janzour mjini Tripoli, hii ikiwa ni kulingana na chanzo katika hospitali wanakotibiwa.

Serikali ya Libya inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa, GNA pamoja na ujumbe wa taasisi hiyo nchini humo, UNSMIL kwa pamoja wamevituhumu vikosi vya mbabe wa kivita Khalifa Haftar kwa kuhusika na shambulizi hilo. Hata hivyo, msemaji wa vikosi vinavyomuunga mkono Haftar Ahmad al-Mismari amekana tuhuma hizo.

Ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa umesema ulipeleka timu ya kuchunguza na waliweza kuthibitisha kwamba ndege iliangusha mabomu manne kwenye eneo hilo, ambalo kulingana na UNSMIL ni eneo linalotumiwa na raia na lisilokuwa na vifaa wala miundombinu ya kijeshi.