1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watoto 12,000 wafa kwa suruwa, utapiamlo

Grace Kabogo
19 Septemba 2023

Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya watoto 1,200 wamekufa kwa ugonjwa wa surua na utapiamlo tangu mwezi Mei kwenye kambi za wakimbizi nchini Sudan.

https://p.dw.com/p/4WYys

Umoja huo umeonya kuwa maelfu ya Watoto watakuwa katika hatari ya kifo ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, kwenye nchi hiyo iliyoharibiwa kwa vita.

Allen Maina, mkuu wa afya ya umma wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) amesema watoto waliokufa walikuwa na umri wa chini ya miaka mitano.

Soma zaidi: Kiongozi wa kijeshi wa Sudan ziarani nchini Uganda

Akitoa taarifa katika Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Maina, amesema watoto hao wamekufa katika kambi tisa katika kipindi cha kati ya Mei 15 na Septemba 14.

Amesema vifo hivyo vimetokana na kuchanganyika wa mlipuko unaodaiwa kuwa magonjwa ya surua na utapiamlo.