Watekaji Nigeria wadai kupewa kitita kuwaachia mateka
13 Machi 2024Watu wenye silaha waliowateka nyara wanafunzi 286 na wafanyakazi kutoka shule moja ya kaskazini mwa Nigeria wiki iliyopita wamedai kupewa kiasi cha naira bilioni moja ambazo ni sawa na dola 620,432 ili kuwaachia huru.
Hayo ni kwa mujibu wa msemaji wa familia za mateka hao, na diwani wa eneo hilo aliyezungumza na shirika la habari la Reuters. Jubril Aminu, kiongozi wa kijiji amesema amepigiwa simu na watekaji nyara hao jana Jumanne.
Amesema walitoa muda wa mwisho wa kulipa fedha hizo katika siku 20, kuanzia tarehe ya tukio hilo la utekaji.
Kwa mujibu wa Aminu, watekaji hao wamesema watawauwa wanafunzi wote na wafanyakazi wa shule kama fedha hizo za kikomboleo hazitatolewa.Jeshi la Nigeria lawasaka waliowateka wanafunzi 300
Wanafunzi hao, pamoja na wafanyakazi kadhaa wa shule walitekwa nyara Machi 7 katika mji wa Kuriga, katika jimbo la kaskazini magharibi mwa Nigeria, la Kaduna. Hilo ndio tukio la kwanza la utekaji nyara wa watu wengi kwa wakati mmoja nchini humo tangu mwaka wa 2021