1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Nigeria lawasaka waliowateka wanafunzi 300

Bruce Amani
11 Machi 2024

Wanajeshi wa Nigeria wanaendelea na operesheni ya kuwasaka watekaji nyara waliowakamata karibu wanafunzi 300 katika jimbo la Kaduna wiki iliyopita.

https://p.dw.com/p/4dOf6
Jeshi la Nigeria
Wanajeshi wa Nigeria wametumwa kwenye jimbo la Kaduna kuwaokowa wanafunzi 300 waliotekwa nyara.Picha: AUDU ALI MARTE/AFP/Getty Images

Chanzo kimoja cha usalama kilisema kuwa vikosi vya kambi ya kijeshi ya Kaduna vinaongoza operesheni hiyo na vilikuwa vinawakaribia wavamizi hao waliokuwa na silaha.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa askari hao walikuwa wanasaidiwa na polisi ya eneo hilo, shirika la upelelezi na jeshi la angani, pamoja na kitengo cha ulinzi wa jimbo la Kaduna, na kundi la walinzi wenyeji wanailofahamu vyema eneo hilo.

Soma zaidi: Wanafunzi 15 watekwa katika kisa cha karibuni zaidi cha utekaji, Nigeria

Msemaji wa gavana wa jimbo la Kaduna, Muhammad Shehu Lawal, alisema vyombo vya ulinzi na serikali ya jimbo walikuwa wanafanya juu chini kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliotekwa wanaachiwa huru.

Jeshi la Nigeria halikutaka kuzungumzia habari hizo kwa sasa. 

ukio hilo la utekaji nyara wa wanafunzi wengi Alhamisi wiki iliyopita ni la kwanza tangu Julai 2021, na limesababisha mshtuko mkubwa katika kijiji cha Kuriga, ambako wazazi wanasubiri majibu kutoka kwa mamlaka.