1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wateka nyara waipa siku 10 Uingereza kuondoa Iraq

5 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CXEg

BAGHDAD.Watekaji nyara wanaowashikilia mateka raia watano wa Uingereza toka mwezi wa Mei wametoa mkanda wa video wakitishia kumuua mateka mmoja iwapo majeshi ya Uingereza hayataondoka nchini Iraq katika kipindi cha siku 10.

Mkanda huo wa video uliyorushwa na kituo kimoja cha televisheni cha uarabuni, umemuonesha mateka huyo akiwa amekaa mbele ya bango la kundi la Shi´ite Islamic Resistance.

Serikali ya Uingereza imelaani kutolewa kwa mkanda huo wa video na bado haijatangaza majina ya mateka hao ambao walitekwa kutoka katika ofisi za wizara ya fedha mjini Baghdad.