1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watafiti wagundua aina sugu ya malaria barani Afrika

Iddi Ssessanga
23 Septemba 2021

Watafiti wamegundua ushahidi wa aina sugu ya malaria nchini Uganda, na kuibua wasiwasi kuwa dawa kuu inayotumiwa inaweza kukosa matumizi iwapo hatua zaidi hazitachukuliwa kuzuwia kuenea kwa vimelea hivyo sugu.

https://p.dw.com/p/40imD
Anopheles Mücke
Picha: David Spears/Ardea/imago images

Watafiti nchini Uganda walichambua sampuli za damu kutoka kwa wagonjwa waliotibiwa na dwa ya artemesinin, ambayo ni dawa ya msingi inayotumiwa dhidi ya malaria barani Afrika kwa kuchanganywa na dawa nyengine.

Waligundua kuwa kufikia 2019, karibu asilimia 20 ya sampuli zilikuwa na mabadiliko ya kimaumbile, hali iliyoonesha kuwa matibabu hayakuwa na ufanisi.

Uchunguzi wa maabara ulionesha ilichukua muda mrefu zaidi kwa wagonjwa hao kuondoa vimelea vinavyosababisha malaria.

Aina za malaria zinazostahimili dawa hiyo ziligunduliwa awali barani Asia, na maafisa wa afya wamekuwa wakifuatilia kwa hofu ishara zozote barani Afrika, ambalo linachangia zaidi ya asilimia 90 ya visa vya malaria duniani.

Aina nyingine sugu za malaria zimeshuhudiwa huko nyuma nchini Rwanda.