1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiIndonesia

Miili mitatu ya wakimbizi wa Rohingya yaokolewa baharini

Lilian Mtono
24 Machi 2024

Miili ya wakimbizi watatu wa Rohingya imepatikana baharini baada ya mamlaka ya Indonesia kumaliza zoezi la kuwatafuta manusura wa ajali ya boti iliyotokea karibu na mkoa wa Aceh.

https://p.dw.com/p/4e4Mk
Rohingya-Wakimbizi wakiwa Indonesia
Wakimbizi wa Rohingya wakiwa wamesimama kwenye boti yao iliyopinduka kabla ya kuokolewa katika maji ya Aceh MagharibiPicha: Reza Saifullah/AP/dpa/picture alliance

Mkuu wa Kikosi cha uokozi kwenye eneo la Banda Aceh Al Hussain amesema walifanikiwa kupata miili hiyo mitatu inayodaiwa kuwa ni wakimbizi wa Rohingya baada ya kupekua eneo la ajali, na kupelekwa hospitalini kabla ya kuzikwa baadae.

Wavuvi na kikosi cha uokozi awali walifanikiwa kuwaokoa watu 75 waliokuwa kwenye boti hiyo siku ya Alhamisi.

Wachache miongoni mwao walipelekwa hospitali iliyoko kwenye eneo hilo, lakini wengi walipelekwa kwenye makazi ya muda yaliyoko kwenye wilaya ya Aceh Barat.