1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapalestina wenye silaha wauwa mtu mmoja Ukingo wa Magharibi

Lilian Mtono
22 Februari 2024

Raia watatu wa Palestina wamewafyatulia risasi watu waliokuwa wamepaki magari karibu na kituo cha ukaguzi katika eneo linalokaliwa na Israel kwa mabavu la Ukingo wa Magharibi.

https://p.dw.com/p/4cjk7
Ukingo wa Magharibi | Polisi wakiwa katika eneo la tukio baada ya shambulio la bunduki
Polisi wa Israel wakipima eneo tukio baada ya shambulio la bundukiPicha: Mahmoud Illean/AP Photo/picture alliance

 Mkasa huo umetokea karibu na mji wa kale wa Jerusalem mapema hii leo na kumuua mtu mmoja na kuwajeruhi wengine watano.

Mkuu wa huduma ya magari ya kubebea wagonjwa nchini Israel Eli Bean ameliambia shirika la habari la umma la Kan kwamba wanawake wawili wamejeruhiwa vibaya. Jeshi la polisi pia limesema maafisa walifanikiwa kuwaua washambuliaji wawili na kumjeruhi mmoja. 

Soma pia:Jeshi la Israel ladaiwa kutekeleza mauaji Ukingo wa Magharibi

Msemaji wa jeshi hilo amesema washambuliaji hao walikuwa ni Wapalestina, ingawa hakutoa maelezo zaidi.

Hali ya wasiwasi tayari imeongezeka katika eneo la Ukingo wa Magharibi kutokana na vita kwenye Ukanda wa Gaza, ambavyo kulingana na Wizara ya Afya inayosimamiwa na Hamas huko Gaza, karibu watu 29,410 wameuawa katika vita hivyo vilivyoanza Oktoba 7.