1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanasiasa wanawake DRC wakabiliwa na changamoto lukuki

Admin.WagnerD19 Mei 2022

Nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, baadhi ya wanawake wanaotarajia kuwa wagombea kwenye uchaguzi unaopangwa kufanyika mwakani wametaja kukabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo kiuchumi na kijinsia.

https://p.dw.com/p/4BaAu
DR Kongo Umweltministerin Eve Bazaiba
Picha: Dirke Köpp/DW

Nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, baadhi ya wanawake wanaotarajia kuwa wagombea kwenye uchaguzi unaopangwa kufanyika mwakani wametaja kukabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo kiuchumi na kijinsia.

Hayo walibainisha  walipokutana mjini Bukavu na wenzao waliokuwa wagombea hapo awali ili kujadili pamoja kuhusu uzoefu wa kisiasa na mbinu za kufaulu kwenye uchaguzi unaopangwa mwaka 2023.

Mkutano huo ulioandaliwa na Jumuiya wanawake wa Congo kwa ajili ya amani ukiwaleta pamoja wanasiasa wanawake na wale ambao watajitosa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu hapo mwakani, ililenga kujadili mikakati ya kuelekea uchaguzi mkuu.

Miongoni mwa changamoto ambazo wameziainisha kuwa ni kikwazo katika kufikia usawa wa kisiasa ambao wanaupigania, ni pamoja na changamoto za kijinsia na kiuchumi.

soma zaidi:DRC yaadhimisha miaka 25 tangu Mobutu alipoondolewa madarakani

Bobilia Nondo Colette ni miongoni mwa wagombea watarajiwa wilayani Fizi,aliiambia DW kwamba ni wakati sasa wa eneo lake kuwa na kiongozi mwanamke kutokana na wengi waliopita ni wanaume, hivyo changamoto za kundi la wanawake zitawasilishwa ipasavyo.

"Fizi kuna viongozi wanawake wachache, nitagombea ili kuwakilisha wanawake wengine" alisema Colette.

Aliongeza kuwa dhima yake ni kuweza kuziwakilisha changamoto za wanawakewa eneo hilo katika kila sekta lakini kinachowaangusha wanawake wengi ni changamoto za kimfumo wanazokabiliana nazo kwenye ulingo wa kisiasa.

Walioshindwa uchaguzi wawapa mbinu

Baadhi ya wanawake ambao walijitosa kwenye chaguzi zilizopita na kushindwa kutokana na kutotosha kwa kura, walisema kuna haja ya wanasiasa hao wanawake kuzingatia ushauri wa wale ambao waliingia kwenye mchakato huo wa kidemocrasia na wanaume na kuwashinda kwenye matokeo ya mwisho.

Kongo Denis Sassou Nguesso
Raia akiwa katika zoezi la upigaji kura DRCPicha: Alexis Huguet/AFP

Soma zaidi:Jules Alingete akosolewa kwa kusema hakuna vita DRC

Walisema ni wakati sasa wa kuweka changamoto zinazowakabili wanasiasa wanawake bayana, ikiwemo kukumbwa na changamoto mbalimbali za kijinsia wakati wa mchakato huo wa kidemocrasia, hatua ambayo wengi imekuwa ikiwakatisha tamaa.

Aidha waliwasisititiza kutozungumza hadharani mbinu zao za ushindi mbele ya wapinzani wao, kwani huko ni kutangaza mbinu za kivita mbele ya mpinzani.

" Rushwa ilikuwa ni kubwa, niwaambie wanawake tupiganie hili kwanza" Alisema Bazilienne Zawadi Bagaya aliekuwa mgombea wa ubunge wilaya ya Babare.

Kundi la wanasiasa wanawake waliofika katika majadiliano hayo walikubaliana kwa pamoja kuhakikisha wanasaidiana na kuelimisha umma kila wanapokuwa katika majukwaa ya kisiasa kuhusiana na masuala ya ujinsia kwenye siasa ili kufikia lengo la hamsini kwa hamsini kwenye nafasi wa uwakilishi.

Uchaguzi wa mnamo mwaka 2018, ni wanawake wagombea watatu pekee waliochaguliwa kwenye bunge la mkoa wa kivu kusini dhidi ya wabunge wanaume arobaini na nne (44), mwanamke mwingine aliteuliwa baadae kuwa mbunge.

Wanawake DRC waanzisha mradi wa kilimo kuwalisha wafungwa