1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

RSF yafanya shambulizi kubwa la droni mashariki mwa Sudan

18 Desemba 2025

Wanamgambo wa RSF wanaopambana na jeshi nchini Sudan, wamefanya Alhamisi shambulizi kubwa la droni mashariki mwa nchi hiyo na kuulenga mtambo muhimu wa kuzalisha umeme.

https://p.dw.com/p/55dyb
Port Sudan | Shambulizi la droni lililofanywa na Wanamgambo wa RSF
Shambulizi la droni la Wanamgambo wa RSF katika mji wa Port-SudanPicha: AP Photo/picture alliance

Kampuni ya kitaifa ya kusambaza ya umeme nchini  Sudan  imesema mashambulizi hayo ya leo ya RSF yamesababisha kukatika kwa umeme katika baadhi ya miji mikubwa ikiwa ni pamoja na mji mkuu, Khartoum na Port Sudan. Abdel Rahim al-Amin, afisa katika jimbo la Port Sudan, ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa, AFP kuwa umeme ulikatika kwenye eneo hilo tangu saa nane usiku.

Katika miezi ya hivi karibuni, wanamgambo wa RSF wamekuwa wakishutumiwa kwa kuyashambulia maeneo makubwa yanayodhibitiwa na jeshi kwa kutumia droni, kuilenga miundombinu ya kiraia na kusababisha kukatika kwa umeme, na hivyo kuwaathiri mamilioni ya watu.