1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanaharakati: Waliouawa nchini Iran ni zaidi ya 3,000

17 Januari 2026

Wanaharakati wa haki za binadamu wamesema leo kwamba zaidi ya watu 3,000 wamekufa katika maandamano ya kitaifa nchini Iran, huku kukiwa na taarifa za kuimarika kidogo kwa matumizi ya mtandao wa intaneti.

https://p.dw.com/p/56z8w
Iraq Najaf 2026 | Mkutano wa makundi ya Washia katika mshikamano na serikali ya Iran
Maandamano ya Washia kuunga mkono serikali ya Iran huko IraqPicha: Alaa Al-Marjani/REUTERS

Wanaharakati wa haki za binadamu wamesema leo kwamba zaidi ya watu 3,000 wamekufa katika maandamano ya kitaifa nchini Iran, huku kukiwa na taarifa za kuimarika kidogo kwa matumizi ya mtandao wa intaneti nchini humo baada ya kuzimwa kwa siku nane.

Kundi moja la HRANA lenye makao yake nchini Marekani limedai kuthibitisha vifo vya watu 3,090, vikiwemo vya waandamanaji 2,885, baada ya wakazi kuripoti kuwa ukandamizaji wa serikali umepunguza kwa kiasi kikubwa maandamano kwa sasa, na kukamatwa kwa watu zaidi.

Wakaazi kadhaa waliozungumza na shirika la habari la Reuters walisema kwamba mji mkuu wa Tehran umekuwa mtulivu ikilinganishwa na siku za nyuma, kwa kipindi cha siku nne mfululizo.

Maandamano hayo yalianza Desemba 28 kutokana na hali ngumu ya kiuchumi, na baadae kugeuka kuwa maandamano makubwa yanayoipinga serikali.