1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanafunzi 11 wa chuo Kenya wafa katika ajali ya barabarani

19 Machi 2024

Wanafunzi 11 wamekufa na wengine 42 wamejeruhiwa baada ya ajali ya basi lililokuwa limebeba wanafunzi wa chuo kikuu nchini Kenya kugongana na lori.

https://p.dw.com/p/4dtNo
Nairobi| Barabara
Moja ya Barabara kuu jijini Nairobi Kenya kuelekea KaskaziniPicha: Tony Karumba/AFP/Getty Images

Wanafunzi 11 wamekufa na wengine 42 wamejeruhiwa baada ya ajali ya basi lililokuwa limebeba wanafunzi wa chuo kikuu nchini Kenya kugongana na lori. Ajali hiyo imetokea jana jioni kwenye barabara kuu yenye shughuli nyingi huko Maungu takriban kilometa 360 kutoka Nairobi.   Idadi ya vifo vya ajali mbaya ya barabarani Kenya yafikia 49  

Wanafunzi hao walikuwa ni kutoka katika Chuo Kikuu cha Kenyatta na walikuwa wakisafiri kuelekea mji wa pwani wa Mombasa. Polisi wamesema kulikuwepo na mvua kubwa ambayo huenda ilisababisha ajali hiyo.

Ajali za barabarani hutokea mara kwa mara katika taifa hilo la Afrika mashariki, ambako hali ya barabara mara nyingi huwa mbaya huku kanuni za uendeshaji zikiwa zinakiukwa au kupuuzwa. Kati ya Januari mosi na Februari 11 mwaka huu, watu 536 walikufa kutokana na ajali za barabarani.