Wakimbizi wa Goma wana hali mbaya | Matukio ya Afrika | DW | 30.05.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Wakimbizi wa Goma wana hali mbaya

Zaidi ya watu 10,000 kutoka vijiji tisa vilivyoshuhudia mapigano wanaishi katika hali mbaya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, huku wakimbizi wakilala nje bila hata mahema, wengine wakikabiliwa na njaa.

A displaced Congolese woman and her young child stand in a crowd of people waiting for humanitarian aid in a camp for the internally displaced in Mugunga, 8km west of Goma in the east of the Democratic Republic of the Congo on November 24, 2012. Tens of thousands of people are displaced in Mugunga alone following fighting between the government army and M23 rebels, who took Goma on Tuesday. AFP PHOTO/PHIL MOORE (Photo credit should read PHIL MOORE/AFP/Getty Images)

Kongo Frauen

Ukitembelea makambi ya wakimbizi, iwe yale yaliyotayarishwa na serikali kwa ajili ya kuwahifadhi raia wanaokimbia vita au majengo ya shule yanayowahifadhi wakimbizi bila ya kutengwa na serikali, utapigwa na bumbuwazi kwa jinsi wakimbizi wanavyoishi kama wanyama.

Katika baadhi za kambi za wakimbizi hakuna mahema, blanketi wala vifaa vya matumizi ya nyumbani. Baadhi ya watoto wameshadhohofika kutokana na kukosa chakula.


Wamoja wao wanalala kwenye mawe ya volkano, na mama zao wakiwa hawana chochote kwa ajili ya mlo kwa watoto wao zaidi ya kulia pamoja na watoto wao wanaoumwa na njaa.

Wakimbizi kwenye kambi ya Kituku katika mji wa Goma wamefikia umbali wa kuomba kurudi makwao , ili wakafie huko katika vita, badala ya kufa kwa njaa na maradhi kutokana na majanga kambini.

Wapiganaji wa M23 kabla ya kuondoka Goma.

Wapiganaji wa M23 kabla ya kuondoka Goma.


Tayari Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na maswala ya kiutu na misaada ya dharura, Bibi Kyung Wang Kang, ametembelea kambi ya wakimbizi ya Sotraki, ambako wakimbizi si chini ya elfu tatu wanajihifadhi. Lakini tangu kufanyika kwa ziara hiyo, hakuna hata shirika moja lililojitokeza kuwasaidia wakimbizi hao.


Vita vya kila mara katika mkoa wa Kivu ya kKaskazini vimesababisha maelfu ya watu kuyahama makaazi yao na kukimbilia kambini, lakini hadi sasa wengi wao hawajui ni siku gani watapata chakula.

Mwandishi: John Kanyunyu /DW Goma
Mhariri: Mohammed Abdulrahman

DW inapendekeza