Wadhamini wamtaka Blatter ajiuzulu maramoja | Michezo | DW | 03.10.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Wadhamini wamtaka Blatter ajiuzulu maramoja

Rais wa Shirikisho la Kandanda Ulimwenguni - FIFA Sepp Blatter amekataa wito uliotolewa na makampuni makubwa wadhamini wa shirikisho hilo ikiwa ni pamoja na Coca cola na McDonald's yaliyomtaka ajiuzulu mara moja

Makampuni hayo yanamtakama Blatter ajiuzulu badala ya kungojea hadi uchaguzi mwingine uliotishwa mwezi Februari mwakani. Rais wa Shirikisho la Kandanda Ulimwenguni - FIFA Sepp Blatter amekataa wito uliotolewa na makampuni makubwa wadhamini wa shirikisho hilo ikiwa ni pamoja na Coca cola na McDonald's yaliyomtaka ajiuzulu mara moja wadhifa huo badala ya kungojea hadi uchaguzi mwingine uliotishwa mwezi Februari mwakani.

Hatua hiyo inakuja wiki moja tu baada ya Rais huyo wa FIFA mwenye umri wa miaka 79 kuanza kuchunguzwa na serikali ya Uswisi kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha ndani ya shirikisho hilo.

Blatter ambaye ameiongoza FIFA tangu mwaka 1998 amekataa hatua ya makampuni hayo akisema kujiuzulu kwake nafasi hiyo katika kipindi hiki hakutaleta tija kwa sasa ndani ya shirikisho hilo.

Makampuni mengine yanayoshinikiza kujiuzulu kwa Blatter ni pamoja na Visa na Budweiser. Visa inasema kuwa hakuna mabadiliko yoyote ya maana yanaweza kufanyika katika kipindi cha usimamizi wa sasa.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Mohamed Dahman