Waasi wadhibiti upya miji muhimu Libya
27 Machi 2011Matangazo
Kwa mujibu wa wizara ya ulinzi ya Marekani mjini Washington, vikosi hivyo vya muungano wa kimataifa, vile vile vimehujumu miji ya Tripoli, Misrata na Ajdabiya.
Waasi wa Libya wakisaidiwa kutoka angani na ndege za muungano huo wa kimataifa, wamefanikiwa kuudhibiti tena mji muhimu wa Ajdabiya.
Ushindi wa wapinzani hao wa serikali ya kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi, unatazamwa kama ni ishara kuwa mapambano ya kuidhibiti nchi hiyo, yanachukua mkondo mpya. Vikosi shirika vya Ufaransa vimesema kuwa vimeteketeza ndege saba na helikopta mbili zilizokuwepo kwenye kituo cha jeshi la anga huko Misrata.