1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Virusi vyaua wanaume wengi kuliko wanawake, Afrika

5 Machi 2021

Utafiti uliofanywa kwenye nchini 28 za Afrika ikiwemo Guinea, Mauritius na Uganda umeonesha kwa wastani idadi ya wanawake waliopata maambukizi au kufa kwa corona ni ndogo ikilinganishwa na wanaume.

https://p.dw.com/p/3qG0s
Angola Corona-Pandemie | Beginn Impfung
Picha: Osvaldo Silva/AFP

Umoja wa Mataifa umesema leo kuwa virusi vya corona vinasababisha vifo vya wanaume wengi zaidi barani Afrika kuliko wanawake ambao kwa sehemu kubwa waandamwa na uwezekano wa kupoteza maisha kutokana na matatizo ya uzazi kuliko Covid-19.

Utafiti uliofanywa kwenye nchini 28 za Africa, ikiwemo Guinea, Mauritius na Uganda umeonesha kwa wastani idadi ya wanawake waliopata maambukizi au kufa kwa corona ni ndogo ikilinganishwa na wanaume.

Takwimu zilizokusanywa zinaonesha kwa wastani asilimia 41 ya wanawake barani Afrika ndiyo wamekumbwa na janga la corona lakini idadi hiyo inatofautina miongoni mwa mataifa.

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa kanda ya Afrika Matshidiso Moeti amesema kwa wanawake janga la covid-19 limesababisha ukosefu wa huduma za uzazi na wengi wanaweza kufariki kwa sababu hiyo kuliko matatizo yanayotokana na virusi vya corona.

Soma Zaidi:Mataifa ya Afrika yahimizwa kuongeza upimaji wa covid-19