ECOWAS yasema inakabiliwa na ukosefu wa usalama wa kikanda
23 Juni 2025
Matangazo
Rais Julius Maada Bio wa Sierra Leone, aliyechukua uwenyekiti wa kupokezana wa Jumuiya hiyo kutoka kwa Rais Bola Tinubu wa Nigeria, alisema Afrika Magharibi inapitia changamoto kubwa.
Niger, Burkina Faso na Mali zaombwa kurejea ECOWAS
Changamoto hizo ni pamoja na ukosefu wa usalama katika kanda ya Sahel na mataifa ya pwani, ugaidi, ukosefu wa utulivu wa kisiasa, upitishaji wa silaha kimagendo na uhalifu wa kupangwa.
Katika mkutano wa viongozi hao uliofanyika jana mjini Abuja, Nigeria, Maada Bio alisema muda umefika wa kushirikiana kikamilifu kiusalama, ikiwemo kuwa na kitengo cha pamoja cha ujasusi na kitengo cha utoaji wa majibu ya haraka.