1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiKenya

Viongozi Afrika washinikiza mageuzi katika mifumo ya mikopo

12 Mei 2026

Viongozi wa Afrika wametumia siku ya pili ya mkutano wao na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kushinikiza mageuzi katika mfumo wa kimataifa wa mikopo na ufadhili.

https://p.dw.com/p/5Dd6u
Mkutano wa Africa Forward 2026 | Macron na Ruto
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Rais wa Kenya William Ruto wakisalimiana wakati wa mkutano wa "Africa Forward 2026"Picha: Monicah Mwangi/REUTERS

Zaidi ya viongozi 30 wa serikali za Afrika wanahudhuria mkutano huo unaofanyika jijini Nairobi, Kenya, unaoitwa Africa Forward—ikiwa ni mara ya kwanza kwa Ufaransa kuandaa mkutano wa aina hiyo katika nchi ya Afrika inayozungumza Kiingereza.

Rais wa Kenya William Ruto amesema, "Sisi kama viongozi wa Afrika tunaelewa kwamba pia tuna wajibu wetu. Uhusiano huu hauwezi kuwa wa upande mmoja. Tunatarajia kutoka kwa Ufaransa kama ambavyo wao watatarajia kutoka kwetu, na wao watatoa kadiri tunavyotoa sisi. Huo ndiyo ushindi wa kweli  kwa pande zote - uhusiano wa manufaa ya pamoja."

Macron ameusifu mkutano huo, akisema umechochea ahadi za uwekezaji wa euro bilioni 23 barani Afrika, akitaja hatua hiyo kama ushahidi wa dhamira ya Ufaransa kujenga uhusiano wa usawa na mataifa ya bara hilo.