1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi mbalimbali kuhudhuria uapisho wa rais wa Taiwan

17 Mei 2024

Viongozi wa mataifa manane watakuwa miongoni mwa wajumbe 51 wa kimataifa watakaohudhuria sherehe ya kuapishwa kwa kiongozi mpya wa Taiwan Lai Ching-te siku ya Jumatatu wiki ijayo.

https://p.dw.com/p/4fyfH
Taiwan, Taipei | Rais mteule Lai Ching-te
Rais mteule wa Taiwan Lai Ching-tePicha: Carlos Garcia Rawlins/REUTERS

Viongozi wa mataifa manane watakuwa miongoni mwa wajumbe 51 wa kimataifa watakaohudhuria sherehe ya kuapishwa kwa kiongozi mpya wa Taiwan Lai Ching-te siku ya Jumatatu wiki ijayo. Haya yamesemwa leo na mamlaka ya kisiwa hicho kinachojitawala.

Viongozi hao wanane ni pamoja na Rais Santiago Pena wa Paraguay, mshirika wa pekee wa kidiplomasia wa Taiwan katika eneo la Amerika Kusini pamoja na mwenzake wa visiwa vya Marshall Hilda Heine, Rais wa Palau Surangel Whipps Jr na waziri mkuu mpya wa Tuvalu Feleti Teo.

Soma: Je, mzozo wa China na Taiwan kuongezeka baada ya uchaguzi?

Wajumbe wengine wa ngazi za juu wakiwemo kutoka Marekani, Japan na Canada, pia watakuwa sehemu ya sherehe hizo kama ishara ya kuunga mkono demokrasia ya Taiwan.

Rais ajaye Lai Ching-te ataapishwa huku kukiwa na ongezeko la shinikizo la kidiplomasia na kijeshi kutoka kwa taifa jirani la China linalodai kuwa kisiwa hicho kinachojitawala ni sehemu ya himaya yake.