1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UgaidiAfrika

Utekaji Nigeria wafikia kiwango cha mzozo

12 Machi 2021

Utekaji nyara wa watu kaskazini mwa Nigeria umekuwa ukifanyika kila mara huku makundi ya kihalifu yakiwachukulia wahanga kama chanzo cha kipato na wanakijiji ambao wamepuuzwa na serikali wamekuwa wakijiona kama takataka.

https://p.dw.com/p/3qWz7
Nigeria Rebecca Samuel Yaga
Picha: Getty Images/AFP/STRINGER

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari alitoa amri ya kuuwawa kwa kufyatuliwa risasi mtu yeyote atakeyeonekana na bunduki katika msitu wowote nchini humo, baada ya kutekwa nyara kwa wasichana 279 wa shule hivi majuzi.

Ofisi yake pia ilisema rais huyo amepiga marufuku shughuli zozote za uchimbaji madini katika jimbo la Zamfara pamoja na marufuku ya kuruka kwa ndege katika anga ya jimbo hilo.

Soma pia: Wanafunzi watekwa tena Nigeria

Makundi ya kihalifu yamezidi kuhusika katika utekaji nyara, ubakaji na matendo mengine ya kihalifu katikati na kaskazini mwa Nigeria. Malengo ya makundi hayo kufanya vitendo hivyo kawaida ni kupata fedha watoto hapo watakapokombolewa.

Tangu ule utekaji nyara wa wasichana 276 wa shule ya Chibok katika jimbo la Borno Aprili mwaka 2014 na kundi la kigaidi la Boko Haram, kumeshuhudiwa msururu wa visa vya wanafunzi kutekwa nyara kaskazini mwa Nigeria.

Nigeria Boko Haram entführt Schüler
Wafuasi wa muungano wa makundi ya kaskazini (CNG) wakiandamana kuishinikiza serikali kuwaokoa mamia ya wanafunzi wa kiume waliotekwa jimboni Katsina, Desemba 17, 2020.Picha: Kola Sulaimon/AFP/Getty Images

Utekaji nyara huo wa wanafunzi kwa wingi kawaida huipelekea jamii ya kimataifa kulaani na kuiwekea shinikizo serikali ya Nigeria.

Rais Buhari ameamrisha usalama kuimarishwa kaskazini mwa nchi hiyo kabla kuanza kwa msimu wa mvua katikati ya mwezi Mei.

Soma pia: Hatimaye wavulana waliokuwa wametekwa Nigeria wakutana na familia zao

Iwapo hatua hii ya Buhari itatekelezwa na usalama urudishwe katika eneo hilo basi wakulima watarudia shughuli zao za kilimo ifikiapo mwezi Mei.

Kiasi kikubwa cha Wanigeria huuwawa vijijini kaskazini mwa nchi hiyo ila visa hivyo haviripotiwi katika vyombo vya habari. Makundi ya wahalifu kwa kawaida huwashambulia watu kutokana na ukosefu wa usalama wa kutosha kutoka kwa polisi na upatikanaji wa silaha kwa urahisi.

Uhalifu huu wa makundi haya ambao hauhusiki kabisa na ugaidi unaofanywa na Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria, ulianza kama mzozo wa wakulima na wafugaji mwaka 2011 na ukazidi kati ya mwaka 2017 na 2018 na kujumuisha wizi wa mifugo, utekaji nyara kwa ajili ya kupata fedha, udhalilishaji wa kingono na mauaji.

Nigeria Polizei
Maafisa wa polisi ya Nigeria wakiwa nje ya mahakama baada ya mshukiwa wa utekaji nyara kufikishwa mahaka ya jimbo la Lagos, Agosti 30, 2017.Picha: Getty Images/AFP/P. Utomi Ekpei

Serikali imepoteza udhibiti

Mkaazi mmoja ameliambia shirika la habari la DW kuwa wahalifu wanawatoza kodi wakulima kwa ajili ya usalama ishara kwamba serikali imepoteza udhibiti wa eneo hilo.

Karibu watu milioni 21 wanaoishi katika majimbo ya Zamfara, Kaduna, Niger, Sokoto, Kebbi na Katsina wameathirika pakubwa.

Soma pia: Lifahamu kundi la Boko Haram

Kulingana na ripoti ya shirika la SBM Intel, makundi ya wahalifu kawaida yanawalenga watu ambao wana uwezo wa kulipa kiasi kikubwa cha fedha za kikombozi lakini pia yanafanya mashambulizi mengi zaidi na kuitisha fedha ambazo si nyingi kwa kila mhanga.

Makundi haya ya wahalifu yanalalamika kwamba serikali kuu na serikali za majimbo zimewatelekeza katika miaka ishirini iliyopita na kusema kulikuwa na vikwazo katika haki za kulisha mifugo.

Video mpya ya Chibok yasambazwa

Kulingana na Shani Shuaibu ambaye ni mwandishi wa habari ambaye hivi majuzi alipewa fursa adimu ya kuingia katika maficho ya makundi ya wakundi halifu katika jimbo la Zamfara, wafugaji hutozwa kodi ya juu zaidi wanapojaribu kuuza mifugo wao na wakati mwengine wanadhalilishwa na polisi na majeshi.

Soma pia: Boko Haram yakiri kuwateka nyara mamia ya wanafunzi

Mtaalam wa usalama Rabiu Adamu alitoa witgo wa mazungumzo ambayo yangepelekea makundi hayo ya wahalifu kupokonywa silaha. Adamu alisema iwapo amani haitopatikana kupitia mazungiumzo basi njia za nguvu zitumike.

Kamishena wa mawasiliano wa Zamfara amekiri kwamba kuleta amani kaskazini mwa Nigeria ni jambo litakalochukua muda.

Chanzo: DW