1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ushauri wa rais Evariste Ndayishimiye kwa Kanisa Katoliki

Amida Issa18 Oktoba 2021

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye alilikumbusha kanisa changamoto linazopaswa kuzishughulikia, zikiwemo za mapadre kujihusisha na vitendo vya usherati.

https://p.dw.com/p/41oEM
Frankreich Kirche l Sexueller Missbrauch in der katholischen Kirche
Picha: Eric Cabanis/AFP

Hapo ni kwenye kanisa kuu la Regina Mundi mjini Bujumbura, wakati wa uzinduzi wa kongamano la baraza la maaskofu wa kanisa katolika. Askof mkuu wa Bujumbura Gervais Bashimiyubusa ambaye alisema kongamano hilo nilakuwakumbusha waumini kuwa wanatakiwa kutangamana.

''Mkutano huu wawakumbusha waumini kuwa watakiwa kutembea pamoja. Ikiwa Waumini viongozi wa kanisa wasifikiri kuwa hawahusiku, na hata raia wa kawaida wasikubali kutengwa. Waumini wa kristo mwatakiwa kutambua kuwa tuko katika meli moja ndipo tunaweza mnaweza kuendelea na kuiendeleza nchi'', alisema Bashimiyubusa.

Rais Evariste Ndayishimiye aliyehudhuria ibada hiyo ya uzinduzi wa kongamano la baraza la maaskofu, alisema katika jamii kanisa linakabiliwa na changamoto kem kem, na kwamba endapo hazitoshughulikiwa basi zinaweza kuathiri Kanisa katolika na kwamba jamii ndio chanzo cha imani.

Soma pia:Mimba za utotoni zaongezeka nchini Burundi

''Miaka hii tunashuhudia ukahaba uliovuka mipaka''

Rais Ndayishimiye alitaka kanisa kushughulikia maadili bora
Rais Ndayishimiye alitaka kanisa kushughulikia maadili boraPicha: Getty Images/AFP/T. Nitanga

''Katika jamii na familia zetu,  utakuta wanandoa hawachangiyi dini, hivyo watoto dini yao, katika jamii wapo vijana walochukuwa muelekeo usio kubalika, tunao utaja kama laana, ni vijana wenye jinsia moja wanao taka kuishi pamoja kama wanandoa.'',alisema Ndayishimiye, kabla ya kuendelea kusema ''Hiyo ni familia inao kuwa imesambaratika, Miaka hii tunashuhudia ukahaba ulovupa mipaka, hadi kwa wanandoa, na viongozi wa kanisa hawajaepuka shutuma hizo. Watoto wamejaa wanao tajwa kutokuwa na wa baba wakati wengi wababa zao ni wakuu wa kanisa''.

Rais Ndayishimiye amesema matamshi yake hayo ni kama  ushauri kwa viongozi wa kanisa ili wajue wapi pakushuhulikia katika mahubiri yao.

Kauli hizo zimesikika wakati kumekuwa na uhusiano mzuri kati ya serikali ya rais Evariste Ndayishimiye na Kanisa katolika  tafauti na ilivyo kuwa kwenye utawala wa mtangulizi wake. Kanisa katolika licha ya kuwa  mkosowaji mkubwa wa serikali, limekuwa na mchango mkubwa katika harakati za maeneleo ya nchi.