Urusi yashambulia miundombinu ya nishati Ukraine
11 Novemba 2025
Matangazo
Urusi imefanya mashambulizi ya droni katika mji wa kusini wa Ukraine wa Odesa hivi leo na kufanya uharibifu kwenye miundombinu ya nishati na usafiri. Gavana wa mji huo Oleh Kiper amesema mashambulizi hayo pia yamemjeruhi mtu mmoja na kuwasha moto mkubwa katika vituo vingi vya nishati.
Katika upande mwingine, Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema katika taarifa ya video kwamba vikosi vyake pia vimechukua udhibiti katika baadhi ya vituo vya treni kusini na katikati mwa mji wa Ukraine wa Kupiansk Vuzlovyi.
Taarifa hiyo ya Urusi imedai kwamba bado vikosi vyake vinaendelea kufanya mashambulizi katika maeneo hayo. Vita vya Urusi nchini Ukraine vyenye zaidi ya miaka mitatu bado vinaendelea licha ya jitihada mbalimbali za kuvimaliza vita hivyo.