1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUrusi

Urusi imekamata wapangaji wanne zaidi wa shambulio la Moscow

1 Aprili 2024

Idara ya usalama ya Urusi FSB imesema watu wanne waliokamatwa jana Jumapili kwa njama iliyoshindwa ya kutenda "ugaidi" walitoa fedha na silaha kufadhili shambulio la kutisha dhidi ya ukumbi wa matamasha mwezi uliopita.

https://p.dw.com/p/4eJri
Ukumbi wa Crocus mjini Moscow ulioshambuliwa
Ukumbi wa Crocus mjini Moscow ulioshambuliwaPicha: Maxim Shemetov/REUTERS

Idara ya usalama ya Urusi FSB imesema katika taarifa leo imewakamata watu hao katika mkoa wa kusini wa Dagestan ambao "walihusika moja kwa moja katika ufadhili na utoaji wa njia za kigaidi kwa watekelezaji wa kitendo cha ugaidi kilichofanyika Machi 22 katika ukumbi wa Crocus mjini Moscow."

Jana Jumapili kamati ya taifa ya kupambana na ugaidi ya Urusi ilisema imewakamata watu watatu waliokuwa wanapanga kutenda mkururo wa uhalifu wa kigaidi.

Soma pia: Macron asema kundi la IS lilitekeleza shambulio la Moscow 

FSB imesema raia wanne wa kigeni wamekamatwa katika operesheni kwenye mji mkuu wa jimbo Makhachkala, na mji wa karibu wa Kaspiysk.