1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Watu 4 washitakiwa kwa kuhusika na shambulio la Moscow

Zainab Aziz
25 Machi 2024

Watu wanne wanaotuhumiwa kufanya shambulizi kwenye ukumbi wa matamasha na kuwaua watu zaidi ya 130 wamefikishwa mahakamani mjini Moscow.

https://p.dw.com/p/4e6Cr
Moscow |
Washukiwa wawili kati ya hao wanne wamekiri kuhusika na shambulio hilo baada ya kufikishwa  mahakamani Picha: Artyom Geodakyan/TASS/IMGAO

Taarifa ya mahakama imesema washukiwa wawili kati ya hao wanne wamekiri kuhusika na shambulio hilo baada ya kufikishwa  mahakamani kwa mara ya kwanza. Watuhumiwa hao walifikishwa kwenye mahakama ya wilaya ya Basmanny ya mjini  Moscow. Mmoja miongoni mwao ana umri wa miaka 19.

Watu wanne washitakiwa kwa shambulizi la Moscow lililouwa zaidi ya watu 130

Watuhumiwa hao wametakiwa kujibu mashtaka juu ya kufanya hujuma ya kigaidi na kusababisha vifo vya watu.

Wakati huo huo Urusi inaendelea kuomboleza vifo vya watu waliouliwa na washirika wa rais Vladmir Putin wanamtaka afikirie kurejesha adhabu ya kifo kwa magaidi na wauaji.