1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Macron asema kundi la IS lilitekeleza shambulio la Moscow

Zainab Aziz
25 Machi 2024

Rais Emmanuel Macron amesema Ufaransa inazo taarifa kwamba magaidi wanaojiita Dola la Kiislamu (IS) ndio waliofanya shambulio kwenye ukumbi wa matamasha mjini Moscow.

https://p.dw.com/p/4e6bP
Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel MacronPicha: Ludovic Marin/Pool/AP/picture alliance

Macron amewaambia waandishi wa habari kwamba nchi yake inazo taarifa za kijasusi kuhusu magaidi wa dola la Kiislamu waliopanga na kuifanya hujuma hiyo.

Kiongozi huyo wa Ufaransa amesema hayo alipowasili kwenye jimbo la Ufaransa, la Guiana, lililopo Amerika Kusini.

Watu 4 washitakiwa kwa kuhusika na shambulio la Moscow

Ameeleza kwamba magaidi hao mara kwa mara wamejaribu kufanya mashambulio nchini Ufaransa na wakati huo huo ameionya Urusi dhidi ya kulitumia shambulio hilo kuitupia lawama Ukraine.

Magaidi waliwaua watu 137 mjini Moscow katika ukumbi huo wa matamasha mnamo siku ya Ijumaa.