Upinzani Kenya wataka Raila atangazwe Rais | Uchaguzi Mkuu wa Kenya 2017 | DW | 11.08.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Uchaguzi mkuu kenya

Upinzani Kenya wataka Raila atangazwe Rais

Upinzani Kenya unaamini mgombea wake Raila Odinga ameshinda urais, ukikataa matokeo yanayoendelea kutangazwa na Tume ya Uchaguzi IEBC yanayomuonesha Rais Uhuru Kenyatta akiongoza katika uchaguzi uliokuwa na mashaka.

Awali waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry, anayeongoza timu ya waangalizi wa uchaguzi katika kituo cha Carter, alisema ana imani na mfumo wa kielektroniki uliotumika katika uchaguzi wa Kenya. Zaidi ya waangalizi 400 wa kimataifa walishuhudia uchaguzi huo wa Jumanne iliyopita.

Kura zinaendelea kuhasebiwa na matokeo kutolewa na IEBC (Getty Images/AFP/L. Tato)

Kura zinaendelea kuhasebiwa na matokeo kutolewa na IEBC

Hata hivyo upinzani unaedelea kudai kwamba uhesabuji wa kura ulikuwa wa udanganyifu baada ya Odinga kusema Jumatano kwamba mtambo wa kielektroniki wa kupigia kura ulidukuliwa na matokeo yalifanyiwa ukarabati. Tume ya IEBC inaendelea kusisitiza kwamba mtambo wake wa kielektroniki wa kupiga kura haujaathiriwa, licha ya majaribio dhahiri ya kutaka kufanya hivyo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com