Upi mustakabali wa siasa za DRC? | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 07.12.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Upi mustakabali wa siasa za DRC?

Rais Felix Tshisekedi wa jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesema atavunja ushirikiano wa kisiasa baina ya muungano wa vyama vinavyomuunga mkono-CACH, na vile vilivyo upande wa mtangulizi wake, rais mstaafu Joseph Kabila-FCC.

Sikiliza sauti 02:17

Ushirikiano huo umekuwa ukiongoza serikali ya Kongo kwa miaka miwili iliyopita, Kabila akilidhibiti bunge, huku Tshisekedi akiwa na mamlaka ya rais. Kutoka mjini Kinshasa Sudi Mnette amezungumza na mwenyekiti wa cha siasa UDPS Peoples, ambacho ni sehemu ya chama kilichogawanyika kutoka kwa UDPS ya sasa ya Tshisekedi, Valentin Mubake kutaka kujua kwanza hicho kilichosemwa na rais kinaweza kutokea.