1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yataka dola bilioni 1 kukabili mzozo wa kiutu Ethiopia

16 Aprili 2024

Umoja wa Mataifa imewaomba wafadhili kujitokeza kusaidia hali mbaya ya mzozo wa kibinadamu unaozidi kuongezeka nchini Ethiopia.

https://p.dw.com/p/4erHN
Umoja wa Mataifa | Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio GuterresPicha: Yuki Iwamura/AP Photo/picture alliance

Umoja huo umeeleza kuwa zaidi ya watu milioni 21 katika taifa hilo la Pembe ya Afrika wanahitaji msaada, ikiwemo chakula.

Kongamano hilo la wafahdili ambalo limeandaliwa kufanyika jioni ya leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa barani Ulaya, linatarajia kuchangisha dola bilioni moja kwa ajili ya misaada kwa miezi mitatu ijayo.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, jumla ya dola bilioni 3.24 zinahitajika mwaka huu pekee ikiwemo ya kuwasaidia wakimbizi wa ndani milioni nne.