1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN kuwaadhibu watakaobainika kuhusika na "ugaidi"

28 Januari 2024

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameapa kuwa Umoja wa Mataifa utamuwajibisha mfanyakazi wake yeyote aliyehusika katika vitendo vya kigaidi.

https://p.dw.com/p/4blLc
Ukanda wa Gaza
Makao makuu ya shirika la UNRWA huko GazaPicha: picture alliance/dpa/APA/ZUMA Press Wire

Guterres ameyasema hayo baada ya kuibuka kwa tuhuma kuwa, wafanyakazi kadhaa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Palestina UNRWA walihusika katika mashambulizi ya Oktoba 7, yaliyofanywa na kudhi la Hamas dhidi ya Israel.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amezisihi serikali kuendelea kutoa ufadhili baada ya mataifa tisa kutangaza kusitisha misaada kwa shirika hilo la Umoja wa mataifa linalowahudumia wakimbizi wa Palestina.

Soma pia: Mahakama ya UN yaitaka Israel kuepusha mauaji ya kimbari Gaza

Mataifa hayo ni Uingereza, Ujerumani, Italia, Uholanzi, Uswisi na Finlanda ambayo yaliungana na Marekani Australia na Canada kusitisha ufadhili huo ambao ni chanzo muhimu cha msaada kwa watu wa Gaza.

Wakati huo huo Wizara ya Afya ya Gaza imesema Jumapili kuwa idadi ya Wapalestina waliouwawa tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na Hamas imefikia watu 26,422. Taarifa ya wizara hiyo imeongeza kuwa takriban watu 165 wameuwawa katika kipindi cha saa 24 zilizopita.