Umwagaji damu waendelea Syria | Matukio ya Kisiasa | DW | 29.10.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Umwagaji damu waendelea Syria

Hadi raia 40 wameuawa hapo jana, (29.10.11), baada ya vikosi vya usalama kufyatulia risasi maandamano ya kudai demokrasia na kuiitaka jumuiya ya kimataifa kuzuia ndege kuruka katika anga ya Syria.

epa02983492 A grab made from a video published by Sham News Network on a social network, shows a Syrian (R) displaying a placard as others protest in Hama, Syria, on 28 October 2011. According to media sources, at least 29 people were killed on 28 October when Syrian security forces fired on anti-government protesters demanding the imposition of a no-fly zone in the country to protect civilians, opposition activists said. EPA/SHAM NEWS NETWORK/HANDOUT BEST QUALITY AVAILABLE. EPA IS USING AN IMAGE FORM AN ALTERNATIVE SOURCE, THEREFORE EPA COULD NOT CONFIRM THE EXACT DATE AND SOURCE OF THE IMAGE HANDOUT EDITORIAL USE ONLY/NO SALES +++(c) dpa - Bildfunk+++

Wapinzani wa Rais Aassad, waitaka jumuiya ya kimataifa kuzuia ndege katika anga ya Syria

Wanaharakati na wakaazi wamesema, waandamanaji kadhaa wamejeruhiwa na mamia wengine wamekamatwa katika umwagaji damu huo mkubwa kabisa, kwenye maandamano yanayoendelea nchini humo, tangu miezi saba, kudai mwisho wa utawala wa miaka 41 wa familia ya Assad.

Kufuatia umwagaji huo wa damu, mawaziri wa nchi za Kiarabu wametuma ujumbe mkali kabisa kwa Rais Assad wakimtaka asitishe mauaji ya raia. Kamati maalum ya Umoja wa Nchi za Kiarabu kuhusu mzozo wa Syria imesema, imepeleka risala ya dharura kwa serikali ya Syria kulalamika kuhusu mauaji ya raia wa Syria yanayoendelea nchini humo.

Saudi Foreign Minister Prince Saud al-Faisal, center, is accompanied by Algeria's representative to the Arab league Abdel Kader El-Hagar, left, during an Arab Foreign Ministers meeting at the Arab League headquarters in Cairo Sunday Oct. 16, 2011 to discuss the possibility of suspending Syria's membership of the league. The Arab League has called an emergency meeting Sunday to discuss whether to suspend Syria, officials said, ramping up the pressure on Damascus to end its bloody crackdown on anti-government protesters. (Foto:Amr Nabil/AP/dapd)

Umoja wa Nchi za Kiarabu umelalamika kuhusu mauaji ya raia Syria

Kamati hiyo, katika taarifa iliyotolewa imesema, ni matumaini yake kuwa serikali ya Syria itachukua hatua kuwalinda raia. Mawaziri wa nchi za Kiarabu wamepanga kukutana na maafisa wa Syria katika mji mkuu wa Qatar, Doha, kesho Jumapili.

Mauaji ya siku ya Ijumaa hasa yalitokea katika miji ya Homs na Hama iliyo kati kati ya nchi. Miezi mitatu iliyopita Rais Assad alipeleka wanajeshi na vifaru katika mji wa Hama kuzima maandamano makubwa. Mji wa Homs ni kitovu cha upinzani unaozidi dhidi ya utawala wa mabavu wa Assad.

Baraza la Taifa la Upinzani la Syria limetoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kuwalinda raia. Baraza hilo halikuomba kuivamia kijeshi Syria lakini waandamanaji barabarani wanazidi kupaza sauti kudai hilo.

 • Tarehe 29.10.2011
 • Mwandishi Martin,Prema/RTRE
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/RtqH
 • Tarehe 29.10.2011
 • Mwandishi Martin,Prema/RTRE
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/RtqH
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com