1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiHaiti

UN: Zaidi ya watu 530 wauawa ndani ya mwaka huu nchini Haiti

21 Machi 2023

Umoja wa Mataifa umesema kwamba zaidi ya watu 530 wameuwawa mwaka huu katika machafuko yaliyofanywa na magenge ya uhalifu nchini Haiti,huku wengi wakiuliwa na walengaji risasi.

https://p.dw.com/p/4P0vV
Haiti
Picha: Ralph Tedy Erol/REUTERS

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na haki za binadamu imesema ina wasiwasi kwamba machafuko mabaya yanaongezeka na kushindwa kudhibitiwa.

Msemaji wa ofisi hiyo Marta Hurtado amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva,Uswisi kwamba mpaka kufikia tarehe 15 mwezi huu wa Machi watu 531 wameshauwawa na 300 wamejeruhiwa wakati 277 wakitekwa nyara katika matukio yaliyohusisha magenge hayo.

Soma pia:  Guterres aomba kikosi cha kimataifa kipelekwe Haiti kuzima uhalifu

Visa hivyo vimefanyika zaidi katika mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince.