1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Umoja wa Mataifa waonya kuhusu hali Sudan Kusini

26 Januari 2026

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wameonya kuwa, hali nchini Sudan Kusini inazidisha hatari ya kutokea kwa "ghasia kubwa dhidi ya raia". Hayo yameelezwa na Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini humo.

https://p.dw.com/p/57QLg
Umoja wa Mataifa umesema Sudan Kusini iko katika hatari ya kuingia katika vurugu dhidi ya raia
Raia wa Sudan Kusini wanaokabiliwa na hali mbaya ya kiutu wakielekea kwenye kituo cha kupokea msaada wa chakulaPicha: Rian Cope/AFP

Taarifa iliyotolewa Jumapili na tume hiyo imeelezea hofu kubwa kutokana na mapigano yanayoendelea huko Jonglei, Kaskazini mwa Juba. Kulingana na ripoti hiyo, mashuhuda kwenye eneo hilo wamesema walishuhudia raia wakikimbilia kujificha kwenye madimbwi yenye maji mengi.

Makamanda wa jeshi wadaiwa kuchochea ghasia dhidi ya raia

Tume hiyo imesema taarifa kwa umma zilizotolewa na makamanda zinazohimiza ghasia dhidi ya raia pamoja na kuwaandaa wanajeshi zinaakisi uchochezi hatari wakati ambapo misingi ya mchakato wa amani tayari imeshadhoofika Sudan Kusini.

Taifa hilo changa zaidi duniani limekuwa likikabiliwa na vita, umasikini na ufisadi mkubwa tangu lilipoanzishwa mwaka 2011. Makubaliano ya kugawana madaraka kati ya Rais Salva Kiir na msaidizi wake Riek Machar yaliingia dosari baada ya Machar kutiwa mbaroni ambapo anakabiliwa na kesi ya uhalifu dhidi ya ubinadamu.