Umoja wa Mataifa kujadili mauaji ya Darfur | Matukio ya Afrika | DW | 21.01.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Umoja wa Mataifa kujadili mauaji ya Darfur

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litafanya mkutano wa dharura Alhamisi kuhusu mapigano ya kikabila ambayo yamesababisha vifo vya karibu watu 200 katika jimbo la Darfur nchini Sudan.

Wanadiplomasia wamesema mkutano huo wa faragha umeitishwa na wanachama watatu wa baraza hilo wasio wa kudumu ambao ni Norway, Ireland na Estonia na wanachama watatu wa kudumu Marekani, Uingereza na Ufaransa.

Makabiliano yaliyozuka kati ya kabila la kiarabu na kundi la jamii ya wasio waarabu la Massalit kwenye eneo la El Geneina yamesabibaisha vifo vya zaidi ya watu 100 na kujeruhi wengine zaidi ya 130.

Serikali ya mpito mjini Khartoum imesema wanajeshi kwenye mkoa huo wa magharibi ambako kuondoka kwa ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kumesababisha wasiwasi kutokea umwagikaji zaidi wa damu.