Ukuta kujengwa Lamu kuwazuia magaidi | Matukio ya Afrika | DW | 13.03.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Ukuta kujengwa Lamu kuwazuia magaidi

Kaunti ya Lamu inataka kuutumia ukuta huo kukabiliana washukiwa wa ugaidi wasiingie kutokea nchi jirani ya Somalia.

Gavana wa Kaunti ya Lamu nchini Kenya, Issa Timammy, amezua mjadala kuhusu mpango wa serikali ya kaunti yake kujenga ukuta kwenye mpaka wa Kenya na Somalia katika juhudi za kukabili ugaidi. Akiuhutubia umma katika ukumbi wa Faza mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu wa 2014 Gavana Timammy alisema ukuta huo wa kilomita thelathini hivi utajengwa kati ya mji wa Ishakani na Ras Kamboni, ambapo mashambulizi ya ugaidi yalishuhudiwa mwezi Julai mwaka jana na kusababisha vifo vya watu takribani 90.

Geoffrey Mung'ou alimhoji Gavana Timammy ambaye alianza kwa kueleza ukuta wenyewe ni wa aina gani hasa.

Kusikiliza mahojiano haya bonyeza alama za spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Geoffrey Mung'ou

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

IJUE DW

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com