1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiAfrika

Ukuaji wa uchumi wa Kenya kufikia asilimia 6.3 mwaka 2024

Lilian Mtono
21 Machi 2024

Uchumi wa Kenya unatabiriwa kukua kwa asilimia 6.3 mwaka huu kutoka asilimia 6.1 ya mwaka 2023, hii ikiwa ni kulingana na Wizara ya Fedha hii leo, ambayo imeongeza kiwango cha makisio yake ya awali.

https://p.dw.com/p/4dz2A
Shamba la maua nchini Kenya
Sekta ya kilimo ni miongoni mwa zile zitakazochangia ukuaji uchumi wa Kenya mwaka 2024. Picha: Zhang Chen/Photoshot/picture alliance

Wizara hiyo ilisema mwezi Februari kwamba ilitarajia ukuaji kwa mwaka huu na mwaka 2023 ungefikia asilimia 5.5, kikiwa ni kiwango cha juu ikilinganishwa na asilimia 4.8 ya mwaka 2022.

Ongezeko hili la mwaka huu pamoja na makadirio hayo ya mwaka uliopita, yamo katika mpango wa kiuchumi wa serikali wa kipindi kitakachokamilika mwishoni mwa mwaka 2027.

Chini ya mpango huo, sekta ya kilimo, biashara ndogondogo na za kati zinatarajiwa kuchangia zaidi kwenye ukuaji huo wa uchumi.