1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yashambulia kituo cha kusafisha mafuta cha Urusi

20 Aprili 2026

Jeshi la Ukraine limeshambulia kituo kikubwa cha kusafisha mafuta cha Urusi katika shambulio la pili ndani ya kipindi cha chini ya wiki moja.

https://p.dw.com/p/5CU4L
Urusi Tuapse 2026 | shambulizi la bandari
Shambulizi la Ukraine dhidi ya bandari ya Urusi ya Tuapse mnamo Aprili 29, 2026Picha: Social Media via REUTERS

Maafisa wa Urusi wamesema shambulio la droni la Ukraine dhidi ya bandari ya Tuapse katika  bahari nyeusi  limesababisha moto mkubwa na kifo cha mtu mmoja, kabla ya moto huo kudhibitiwa saa chache baadae.

Gavana wa eneo hilo la Tuapse Veniamin Kondratiev, amesema shambulio hilo limefanya uharibifu mkubwa ndani dhidi ya majengo kadhaa  kote mjini humo ikiwa ni pamoja na shule ya msingi, majengo ya makazi, chekechea, jumba la makumbusho na kanisa.

Wizara ya ulinzi ya Urusi pia imeripoti kudungua droni 112 za  Ukraine usiku wa kuamkia leo.

Katika hatua nyingine, Urusi imesema leo kuwa imemkamata mwanamke mmoja raia wa Ujerumani aliyepatikana na bomu la kujitengenezea, kwenye mkoba wake katika kile kinachodaiwa kuwa njama iliyopangwa na Ukraine ya kulipua kituo kimoja cha usalama kusini mwa nchi hiyo.

Urusi imewakamata watu kadhaa katika vita vyake vya miaka minne nchini Ukraine, wengi wao raia wake yenyewe, kwa madai ya kuifanyia kazi Ukraine.