1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhalisia wasambaratisha uongo wa Trump kuhusu corona

Ines Pohl
2 Oktoba 2020

Amedhihirisha kutotaka kuvaa kabisaa barakoa na amekuwa akipuuza hatari ya janga la ugonjwa wa Covid-19. Lakini sasa rais wa Marekani Donald Trump ameambukizwa mwenyewe, na hii itaathiri uchaguzi ujao, anasema Ines Pohl.

https://p.dw.com/p/3jLoT
Washington US-Präsident Trump
Picha: Joshua Roberts/Reuters

Kwa miezi kadhaa Trump amepuuza hatari za ugonjwa wa Covid-19, kuwakejeli watu wanaojaribu kujilinda kwa kuvaa barakoa, kuutaja ugonjwa huo hatari kama ulioletwa na chama cha Democratic, na kudai kwamba hali si mbaya kihivyo.

Ingawa siyo rahisi kueleza mapema baada ya kutangazwa kwa matokeo ya vipimo, iwapo na kwa namna gani rais huyo mwenye umri wa miaka 74 ataugua, athari za kampeni ya kisiasa ziko wazi sana wakati uchaguzi ukikaribia: Itakuwa janga.

Bila kujali hasara

Majaribio yote ya kuondoa nadhari kwenye kushindwa kwake, ukweli kwamba hakuna mkakati wa kitaifa wa kuwalinda raia, kwamba magavana wameachwa peke yao na wakati huohuo zaidi ya Wamarekani laki mbili wamefariki kutokana na ugonjwa huo, yote hayo yamekuwa batili.

Soma pia: Viongozi wa dunia wamtakia afueni Trump

Uhalisia umesambaratisha uongo wote wa rais. Yeye pamoja na maafisa wake hawatafanikiwa tena  kuwasha mishumaa ya moshi, katika kuyawasilisha maandamano ya vurugu kwenye baadhi ya miji kuwa hatari zaidi ya ukweli kwamba Wamarekani 1000 hufa kila siku kutokana na virusi hivyo.

Pohl Ines Kommentarbild App
Mwandishi wa DW mjini Washington Ines Pohl.

Kwa nguvu zake zote na bila kujali hasara, Donald Trump amejaribu kuufufua uchumi kabla ya siku ya uchaguzi. Kwa tukio hili la kuambukizwa virusi, mpango huu pia umekuwa batili. Hata wakanushaji wa corona hawataweza sasa kuepuka kukiri kwamba virusi hivyo vina uwezo mkubwa wa kusambaa - ikiwa vimeweza kumfikia hata mtu mwenye nguvu aliyoko ikulu ya White House. Oktoba 2, nchi hiyo iko mbali kuliko wawati wowote ule, na utulivu  ambao Trump amekuwa akihaha kuuwekea matumaini.

Soma pia:Maoni: Trump aongeza joto kwa kupendekeza kusogeza uchaguzi 

Nadharia za uovu na njama

Mara baada ya habari za maambukizi yake kuwekwa hadharani, wimbi la taarifa za kumtakia shari rais huyo limeenea, hadi kufikia dhana kwamba  maambukizi hayo ni njama aliyoibuni ili kuondoa nadhari kwenye uchunguzi wa maoni ya wapigakura unaoonesha kushuka vibaya kwa umaarufu wake.

Soma pia: Trump na mkewe waambukizwa virusi vya corona

Anaweza kushughulikia haya. Rais huyo amezowea kuwa na ukweli mbadala. Lakini siyo na kupoteza sifa yake ya askari shupavu. Kwa sababu hiyo inamaanisha hakuna mengi aliyobakisha.

Biden ghafla siyo mzee tena, bali muangalifu

Baada ya mdahalo wa kwanza wa televisheni, hoja kuu ya wafuasi wa Trump ilikuwa kwamba yeye ni imara zaidi na hivyo ndiye anafaa kwa ofisi ya rais inayochosha kuliko mpizani wake. Ikiwa Joe Biden pia hakuambukizwa wakati wa mdahalo huo, hoja hii - alau kwa wiki zijazo, haitakuwa tena na mashiko. Sasa siyo tena udhaifu wake utakaotumiwa, bali busara zake kuhusu umri wake, ambao unaelezwa kwa tahadhari.

Soma pia: Harris atokea kwa mara ya kwanza kwenye kampeni

Trump dhaifu hana kingine zaidi cha kutoa. Na bila shaka siyo kiongozi sahihi wa kupambana dhidi ya janga hatari la maambuzi. Uungwana unatulazimu tumtakie Trump na mke wake Melania kila la kheri katika siku zijazo.