Shule moja Kaskazini mwa Uganda imeamua kuwapa fursa wasichana waliobeba mimba wakiwa shuleni, kurudi tena shuleni na kusoma kama kawaida na wanafunzi wenzao. Hatua hii imewarejeshea matumaini mabinti hao, ambao vinginevyo, kubeba mimba kungekuwa kikomo cha safari yao kielimu. Mwandalizi ni mandishi wetu wa Kampala, Lubega Emmanuel.