Uganda kushiriki michezo maalum ya Frisbee | Michezo | DW | 06.03.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Uganda kushiriki michezo maalum ya Frisbee

Uganda itakuwa timu ya Kwanza ya Afrika mashariki kushiriki katika michezo ya fukwe ya bahari unaofahamika kama Frisbee katika mashindano yatakayoandaliwa nchini Dubai mwezi huu wa Machi

Chama cha michezo hiyo nchini Uganda - Ugandan Ultimate Frisbee Association- (UUFA) kimetangaza kitatuma timu kwenye michezo ya ubingwa wa dunia ya fukwe ya bahari, World Ultimate Beach championship itakayofanyika mwezi huu huko Dubai, Umoja wa Falme za kiarabu..Michezo hiyo huchezwa na mamilioni ya watu duniani, ikiwa ni pamoja na kandanda, mpira wa wavu, rugby na netiboli (netball).

Nchini uganda michezo hiyo inayojulikana kama Frisbee ilianzishwa mjini Kampala 1995, baada ya marafiki fulani kuanzisha mchezo wa kutupiana kisahani cha plastiki kutoka masafa fulani kila jumapili na 1999 na 2000, kikundi kilichoongozwa na Alex Matovu kikaanzisha kilabu maalum katika mji mkuu wa kampala. tayari kuna vilabu vya aina hiyo katika miji ya Makaka, Fort Portal, Bushenyi, Gulu na Luwero. pamoja na kutokuwa na fukwe ya bahari mjini Kampala michezo hiyo hufanyika kila Jumatano na Jumapili jioni katika Chuo kikuu cha Makerere

Mwandishi: Mohammed Abdulrahman
Mhariri: Josephat Charo

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com