1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Ufaransa yatuma wanajeshi zaidi kuzima vurugu New Caledonia

17 Mei 2024

Mamia ya wanajeshi na polisi wa ziada wamewasili katika kisiwa cha bahari ya Pasifiki kilicho chini ya milki ya Ufaransa cha New Caledonia, kufuatia machafuko ambayo yamesababisha vifo vya watu watano.

https://p.dw.com/p/4fxtN
Ghasia kisiwani New Caledonia
Gari ikiwaka moto katika ghasia za New CaledoniaPicha: Delphine Mayeur/AFP

Mamia ya wanajeshi na polisi wa ziada wamewasili katika kisiwa cha bahari ya Pasifiki kilicho chini ya milki ya Ufaransa cha New Caledonia, kufuatia machafuko ambayo yamesababisha vifo vya watu watano huku mamia ya wengine wakijeruhiwa.

Mapema leo Ijumaa, taarifa ya ofisi ya serikali ya Ufaransa katika kisiwa hicho imefahamisha kuwa hali ya dharura imewezesha vikosi vya usalama kurejesha "hali ya amani na utulivu" karibu na mji mkuu Noumea kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa machafuko hayo siku ya Jumatatu.

Ufaransa yapeleka wanajeshi New Caledonia kuzima ghasia

Ghasia hizo zimechochewa na mageuzi ya katiba yanayoshinikizwa na Ufaransa kwenye kisiwa hicho kinachoendesha harakati za kutaka kujitenga. New Caledonia ni kisiwa ambacho kinapatikana kiasi kilomita 1,500 kutoka Mashariki mwa Australia na kina wakazi karibu 270,000.