1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUfaransa

Ufaransa kuondoa dharura kwenye kisiwa cha New Caledonia

27 Mei 2024

Ufaransa itaondoa hali ya dharura katika kisiwa chake cha New Caledonia baada ya siku 12. Haya yametangazwa na afisi ya Rais Emmanuel Macron mjini Paris.

https://p.dw.com/p/4gKCM
Polisi wa Ufaransa
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema vikosi vya usalama vitasalia katika kisiwa chake cha New Caledonia kilichokumbwa na machafuko hivi karibuniPicha: Julien Mattia/AA/picture alliance

Kulingana na vyombo vya habari nchini Ufaransa, hatua hiyo iliyochukuliwa Mei 15 kufuatia machafuko kuzuka katika eneo hilo, haitorefushwa tena na sasa itafikia mwisho kesho Jumanne.

Serikali ya Ufaransa inatarajia kwamba hatua hiyo itachochea kufanyika kwa mazungumzo. Ufaransa pia imetangaza kupeleka polisi wa ziada 480 na kufikisha idadi ya maafisa wa ulinzi wa Ufaransa huko New Caledonia kufikia 3,500.

Ingawa kuna utulivu kwa kiasi kikubwa sasa, uwanja wa ndege katika Mji Mkuu Noumea ambao ulifungwa tangu Mei 14, utaendelea kufungwa na hakuna ndege zitakazoruka hadi angalau Juni 2.

Maandamano yaliyofanywa na makundi ya wadai uhuru kwenye kisiwa hicho kilicho chini ya milki ya Ufaransa yalichochewa na mapendekezo ya mabadiliko ya katiba yaliyopangwa kufanywa na serikali mjini Paris.