1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

India yapiga kura kwa awamu ya tano katikati mwa joto kali

Sylvia Mwehozi
21 Mei 2024

Awamu ya tano ya upigaji kura katika uchaguzi wa India iliendelea jana Jumatatu huku maeneo kadhaa ya nchi hiyo yakikumbwa na wimbi kubwa la joto kali.

https://p.dw.com/p/4g59y
Wapiga kura wa India
Wapiga kura wa IndiaPicha: Satyajit Shaw/DW

Awamu ya tano ya upigaji kura katika uchaguzi wa India iliendelea jana Jumatatu huku maeneo kadhaa ya nchi hiyo yakikumbwa na wimbi kubwa la joto kali. Awamu ya tano ya upigaji kura inayajumuisha maeneo ya bunge 49 katika majimbo sita na maeneo mawili ya vyama vya wafanyakazi.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi anatarajiwa kushinda kwa muhula wa tatu, lakini idadi ndogo ya wapiga kura waliojotokeza, imeibua wasiwasi kwa chama chake cha BJP. Chama hicho kinaonekana kukabiliwa na upinzani mkali kuliko ilivyotarajiwa katika baadhi ya majimbo.

Mamilioni ya watu katika majimbo takribani manne walipiga kura chini ya joto kali linalofikia nyuzi joto 40 katika kipimo cha Celsius.

Uchaguzi wa India unafanyika kwa awamu saba ikiwa ni zaidi ya wiki sita.