Ubelgiji wawaadhibu Panama | Michezo | DW | 19.06.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Ubelgiji wawaadhibu Panama

Ubelgiji wameanza kampeni yao ya kombe la dunia kwa ushindi walipowalaza Panama 3-0. Magoli ya kipindi cha pili kutoka kwa Dries Martins na mawili kutoka kwa mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku yalitosha.

Hao Red Devils kama wanavyoitwa kwa jina la utani Ubelgiji, sasa wana alama tatu muhimu. Kabla ya mechi hiyo Sweden walikuwa wanakwaana na Korea Kusini na wao nao walihakikisha kwamba wanaanza Kombe la Dunia kwa ushindi, walipowatandika 1-0. Andreas Granqvist ndiye aliyewapa Sweden baohilo la ushindi na kuhakikisha kwamba wako kileleni kwenye kundi lao sawa na Mexico. Sweden watachuana na Ujerumani katika mechi yao ya pili ya kundi huku Ujerumani ambao ndio mabingwa watetezi wakitakiwa kutoa ushindi kwenye mechi zao mbili zilizosalia ili wafuzu kwenye ungwe ya muondoano.

Mwandishi: Jacob Safari/APE/DPA

Mhariri: Bruce Amani

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com