1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UAE yazuia makombora kutoka kwa waasi wa Houthi

Saumu Mwasimba
24 Januari 2022

Umoja wa Falme za Kiarabu umesema umezuia makombora mawili ya kasi yaliyodaiwa kufyetuliwa na waasi wa Kihouthi wa Yemen kuelekea anga ya Abu Dhabi.

https://p.dw.com/p/45zzq
Yemen Huthi Kämpfer
Picha: Hani Mohammed/AP Photo/picture-alliance

Maafisa wamesema hilo ni shambulio la pili katika kipindi cha wiki moja ambayo yameulenga mji mkuu huo wa Umoja wa Falme za kiarabu.

Shambulio hilo la kurushwa makombora linazidisha mivutano katika eneo hilo la ghuba ya uajemi ambalo limeshuhudia mkururo wa hujuma karibu na Emarati lakini hazikuwahi kuingia katika ardhi yake, kufuatia vita  vya Yemen vya miaka kadhaa pamoja na kuvunjika makubaliano ya Nyuklia ya Iran na nchi zenye nguvu.

soma zaidi: Umoja wa Mataifa walaani mashambulizi yaliyouwa watu 70 Yemen

Picha za video zilizorushwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii zimeonesha anga ya Abu Dhabi ikigubikwa na mwanga mkali  kabla ya alfajiri katika kile kilichoonekana kama tukio la kudunguliwa kwa makombora.

Waasi wa Kihouthi leo wametishia kuongeza mashambulizi yao dhidi ya Umoja wa falme za kiarabu.