Tunisia yatoa hukumu ya kifo juu ya chapisho la Facebook
4 Oktoba 2025
Matangazo
Katika taarifa kwenye Facebook, Bouthelja amesema kuwa mteja wake ambaye hakutajwa jina, alikuwa kizuizini tangu Januari 2024, kabla ya kesi kuanza. Amesema mshtakiwa ni baba wa watoto watatu na mfanyakazi wa kutwa anayeishi na ulemavu uliosababishwa na ajali iliyotokea kazini mwake.
Mshtakiwa hana ushawishi mkubwa wa mitandao
Bouthelja amesema mteja wake ana kiwango duni cha elimu na asiyekuwa na ushawishi mkubwa mtandaoni.
Uamuzi huo ni wa hivi karibuni zaidi kutumia Amri ya 54, sheria inayoifanya haramu kutayarisha, kueneza, kusambaza, kutuma au kuandika habari za uongo kwa lengo la kukiuka haki za wengine, kudhuru usalama wa umma au ulinzi wa taifa au kuzusha hofu miongoni mwa watu.