Tanzania: Tume ya Jaji Chande yawasilisha ripoti yake
23 Aprili 2026
Matangazo
Miongoni mwa mambo makuu yaliyotangazwa na mkuu wa tume hiyo Jaji Mstaafu Mohammed Chande, ni kuwa idadi ya waliouawa wakati wa ghasia hizo ni 519, na waliojeruhiwa ni zaidi ya 2000.
Thamani ya mali zilizoharibiwa yatajwa
Aidha, thamani ya mali iliyoharibiwa ni shilingi bilioni 125 za Tanzania. Ingawa ripoti haikuelekeza lawama za wazi upande wowote, imesema kuhusu uwezekano wa kutokea kwa matumizi mabaya ya silaha na kutaka uchunguzi wa kina ufanyike.