1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump akubali mchakato wa kukabidhi madaraka kwa Biden

Sylvia Mwehozi
24 Novemba 2020

Idara ya serikali ya Marekani inayoratibu shughuli ya kubadilishana madaraka, imempatia rais mteule Joe Biden idhini ya kuendelea na mchakato wa kukabidhiana madaraka huku Trump naye akionekana kukubali kutoa ushirikiano

https://p.dw.com/p/3ljlb
USA Wilmington | Pressekonferenz Joe Biden nach Videokonferenz mit National Governors Association
Picha: Biden Transition/CNP/MediaPunch/picture alliance

Serikali ya shirikisho imemtambua Rais mteule Joe Biden kuwa "mshindi dhahiri" wa uchaguzi wa Novemba 3, na hivyo kuanza rasmi mchakato wa kubadilishana madaraka baada ya rais Donald Trump kutumia wiki kadhaa ya kuijaribu demokrasia ya Marekani.

Mkuu wa idara inayoratibu shughuli za kubadilishana madaraka GSA Emily Murphy, ameandika barua na kutoa idhini kwa Biden kushirikiana na idara za shirikisho kuelekea siku muhimu ya uapisho Januari 20. Trump amekiri kuwa umefika muda sasa kwa taasisi hiyo kufanya "kinachohitajika" na kaandika katika Twitta kwamba ameielekeza timu yake kutoa ushirikiano katika mchakato wa kukabidhiana madaraka. Hata hivyo Trump amekataa kukubali matokeo hayo akisema ataendelea kupambana mahakamani. Maafisa wa juu Marekani wasema uchaguzi ulikuwa salaama

Katika barua yake Murphy ameandika kuwa hajashinikizwa na mtu au taasisi yoyote, bali maamuzi yake yametokana na "maendeleo ya hivi karibuni yanayojumuisha michakato ya kisheria na udhibitisho wa matokeo ya uchaguzi". Jimbo la Michigan hapo Jumatatu lilithibitisha ushindi wa Biden na jaji wa shirikisho huko Pennyslvania alitupilia mbali kesi ya timu ya kampeni ya Trump siku ya Jumamosi iliyokuwa ikijaribu kuzuia uthibitisho wa matokeo.

USA | Joe Biden und Anthony Blinken
Biden na Antony Blinken mshauri wake wa muda mrefuPicha: Mike Coppola/Getty Images

Hatua ya sasa inamaanisha kwamba timu ya Bidenitaweza kupatiwa fungu, ofisi ya kuratibu shughuli ya kukabiadhana madaraka na uwezo wa kukutana na maafisa wa shirikisho. Ofisi ya Biden ambayo hapo awali ilitangaza kundi lenye uzoefu mkubwa katika uteuzi wa nafasi za wizara za mambo ya nje na usalama, ilisema kwamba Idara ya GSA sasa itatoa"msaada unaohitajika kutekeleza makabidhiano ya amani ya madaraka".

Biden anaonekana kuwa atawateua maafisa wa enzi ya utawala wa Obama kwa ajili ya wizara za usalama na uchumi, ikiashiria mabadiliko amkubwa kutoka serikali ya Trump iliyokuwa ikikumbatia sera za "Marekani kwanza" na kuupa kisogo ushirikiano wa kimataifa.

Miongoni mwa wanaotajwa ni waziri wa zamani wa mambo ya nje John Kerry anayeweza kupewa jukumu la mapambano ya mabadiliko ya tabia nchi, mshauri wa muda mrefu Antony Blinken kuwa waziri wa mambo ya kigeni, mwanasheria Alejandro Mayorkas kuwa waziri wa mambo ya ndani na Avril Haines kama mwanamke wa kwanza kuwa mkuu wa idara ya usalama. Biden pia anatarajiwa kumteua Janet Yellen ambaye atakuwa mwanamke wa kwanza kuongoza wizara ya fedha na Linda Thomas-Greenfield kuwa balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa.