1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TI yaonya kuhusu ufisadi katika kandanda

20 Novemba 2015

Ripoti ya uchunguzi uliofanywa na Shirika la Kimataifa la kuangalia mambo ya rushwa, la Transparency International – TI imesema jumla ya mashirikisho 168 kati ya 209 wanachama wa FIFA hayaweki wazi ripoti zao

https://p.dw.com/p/1H9hW
Logo Transparency International

Mkurugenzi mkuu wa TI Cobus de Swardt amesema katika taarifa kuwa hatari ya ufisadi katika mashirikisho mengi sana ya kandanda ulimwenguni ni kubwa.

Uchunguzi huo unafuatia upelelezi wa uhalifu ulioanzishwa na waendesha mashtaka nchini Marekani na Uswisi dhidi ya FIFA na maafisa wakuu wa kandanda. TI imependekeza kuwa uchunguzi wa mpana wa fedha unapaswa kuwa sehemu muhimu ya kubadilisha utamaduni wa FIFA na wanachama wake.

Ni wanachama 14 pekee – wakiwemo England, Italia, na mashirikisho yote matatu ya Scandinavia – yanayochapisha habari chache inayopendekezwa na TI. Tatu tu kati ya 14 ni wa nchi ya Ulaya: Canada, Japan na New Zealand.

Zaidi ya moja kati ya tano ya mashirikisho 209 ya kitaifa ya kandanda hayana tovuti ya kueleza kazi zao, na 178 hayachapishi ripoti ya kila mwaka ya shughuli zake

Mwandishi: Bruce Amani/DPA/AFP/AP/Reuters
Mhariri:Yusuf Saumu